HADI  tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. 

Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720.
 Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. 

Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Endeleza kampeni CCM ni kuwatakia tu ushindi wa kishindo.

    ReplyDelete
  2. Hadi jana Tarehe 16. Leo ndo tarehe 16 kuna kosa la uandishi au?

    ReplyDelete
  3. Kwa kuwa hiyo tathmini mmeifanya ninyi wenyewe mnaweza kuipamba kwa aina yoyote ile inayo wapendeza. Intellectuals na wataalamu wa polls huwa wanasikiliza zaidi independent pollster au institutions. Sasa kinacho wadhuru ninyi ni ukweli kwamba hampendi tabiri zilizo huru zifanyike. Sasa huna haja ya kutoa matokeo haya kwenye jamii. Ungetuma kwa wana CCM wenzio ili muendelee kujipa false hopes.
    Wananchi wanasikiliza polls za asasi zilizo huru, sio hizi ambazo unaleta hapa. No where on earth CCM will get over 50% of votes in next election. Kikwete on his second term hakufikisha hizo asilimia unazotaja kwenye assesment yako.
    Jidanganye mwenyewe na wachache wenzio.
    Tanzanians are determined, and ready to proves you wrong.

    ReplyDelete
  4. Hata tabiri zilizohuru zikiuliza watu elfu moja wakati tuko milioni arobaini hazina uwakilishi wa ukweli wala sayansi yoyote katika nchi hii ya watu wenye uelewa na ushabiki usiosimamia itikadi. Hukuna cha independent pollster wala nini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...